Sunday, January 2, 2011

VIONGOZI WALA RUSWA NI KAMA KIBAKA AMBAKAE MAMAE.

Hivi kweli mtu unaaminiwa na wanyonge ambao wengi wao wana elimu ya wasiwasi ya darasa la saba, wamekupa dhamana ya kuwaongoza halafu badala kuangalia masilahi yao unaamua kuangalia masirahi yako tu. Watu wenye uchoyo wa mali na wasio kuwa na huruma juu ya wanyonge masikini wana kuja kwako kwa vile wanajuwa dhamana uliyo nayo wanakuja wana kundanganya kwa kukupa vizawadi vidogo ambavyo kwako vinaonekana vikubwa. Basi wewe uzalendo una kushinda una wambia waje ndani ya nchi yako wachukuwe wanacho kitaka halafu wakisha chukuwa wanacho taka wandoke zao wakatengeneze waliko toka au wakanufaishe familia zao kwa maisha ya anasa. kipindi cha dhamana kikiisha unarudi kwa wanyonge unatumia vizawadi ulivyo pewa kuwalaghai wanyonge ili wakupe dhamana nyingine ili uzidi kupewa vizawadi vigine. Miaka nenda rudi mchezo ni huo huo na wewe kutakana na upeo mdogo wakutona mbali unashindwa kujuwa kuwa itafikia kipindi ambapo nchini mwako kutakuwa hakuna kitu cha kuiba basi hao walikuwa wanakupa hivyo vizawadi hautawaona tena. Basi hapo ndio utakapo sema nigelijuwa nagekuwa mwaminifu kwa wananchi wangu isinge kuwa kama ilivyo sasa. Lakini siku zote nigejuwa ina kuja badaye. Hii sio tu kwa viogozi bali hata kwa wafanyakazi wegi wanatumi nafasi walizo nazo kutafuta mpato yasiyo kuwa ya haki. Jamani watu tubadilike tuwe watu wa kujali haki za wasio juwa kudai haki zao.

No comments:

Post a Comment