Wednesday, May 5, 2010

kwanini tunakuwa nyuma siku zote

unajuwa wakati mwingine mimi najiuliza kwanini tanzania tuko nyuma kimaendeleo ingawa nchi yetu imebarikiwa kwa kwa mali asiri nyingi: sio tu madini bali hata aridhi yenye lutuba, nafikiri tanzania inashika namba katika nchi zena alidhi zuri. Pamoja nahayo bado watanzania wengi ni masikini. Kweli tunapaswa kujiliza tatizo liko wapi? Kwa ufupi naweza kusema chanzo kikubwa cha matatizo ya watazania kiko mikononi mwao wenyewe, maana mtu huwezi kufanya kitu kimaja miaka nenda rudi ukategemea kwamba matokeo yatakuwa tafauti. Kwa mfano mtu unalima shamba la eka moja kila mwaka na unapanda maharegwe harafu unategemea kwamba siku moja hilo shamba lako litakuja kukupa mahitaji yako ya mahindi, mchele, nguo na kadharika. Nia yangu sio kuwadharau watanzania kwamba ni wachovu wa mawazo ila nichataka kuonyesha hapa nikwamba watazania kwa ujumula kuazia viogozi wa juu hadi mwanachi wa kawaida kama wanasiasa wetu wanavyo tuita sisi wakulima wa jembe la mkono kwamba ni wananchi wakawaida, tunahitaji kukaa chini natujiulize ni kipi tunakosea kwani nidhahili kuwa kwamba tulicho kuwa tunakifanya kwa miaka mingi sasa sio sahihi. Kwamaana hiyo tubadili mbinu zetu za kuleta maendeleo au tukubali kuwa umasikini ndio staili ya maisha tulio ichagua.