Wednesday, December 15, 2010

maisha ni mazuri hata kama ni ya shida

mara nyingi katika maisha ya kila mtu kuna wakati ambapo kila kitu kinakuwa kama kilivyo pagwa. Nakuna wakati mwingine mtu unaona kama kila kitu katika maisha yako hakiendi sawa. Nahapo ndipo mtu usipo kuwa makini unaweza ukafanya maamuzi ambayo badala ya kurekebisha hali yanafanya hali kuwa mbaya zaidi. kwa maana hiyo mtu unapoona kwamba kuna mkazo wa mambo (stressing situation) nivuzuri ukae chini utulie na ujulize ni tatizo gani linalo nisababishia stress, na kitu gani naweza kufanya ili kubadisha hali hiyo. Jee kunakitu ambacho kipo ndani ya uwezo wangu kinachoweza kurekebisha hali? au ni msaada gani nahitaji ili nirudi katika hali ya kawaida? jee nikweli kila kitu kinayumba katika maisha yangu? kama kila kitu kinayumba jee ni kipi na kipi haswa kinacho yumba. (be specific on these questions)
hili ndio waza la leo. Kama unaswali lolote tafadhali usisite kuniandikia kuppitia( emanubita@gmail.com)

Saturday, June 26, 2010

Blogger Buzz: Blogger integrates with Amazon Associates

michuziblogspot.com

bongoradio.com

hatakama umeukana utanzania bado wewe ni mtanzania

sasa tuna weza kuwekeza au kurudi kutowa changamoto nyumabani tanzania bila kisingizio kwamba oh mimi sio mtanzania tena. tanzania sasa iko kwenye process ya kupitisha sheria ya kuwa na uraia wa nchi mbili. Lakini swali ni kwamba hivi kweli watanzania wanao ishi nchi za nje wako tayari kurudi nyumbani kuwekeza au kutowa chagamoto kwa watanzania ambao hawajawahi kuwa na nafasi ya kutoka nje ya nchi? Mimi naamini kama watanzania wanao ishi nchi za nje wanao nafasi nzuri ya kuleta maendeleo tanzania kama wakiamua kubadilika na kujuwa kwamba nyumbani ni nyumbani hata kama kuna vumbi. wantazania wengi ambao hawajawahi kuishi nje ya nchi bado wana imani potofu kwamba wageni ni bora kuliko wenyeji. Kwa mfano mtu unakuta mhudumu anaona amuhudimie vuzuri mzungu kuliko mtazania mweusi. Mfano mzuri ni pale airport Dar ukitaka usisumbuliwe na wafanyakazi wa airport ni bora usiogea kiswahili ujifanye wewe ni mgeni ndio utahudumia vuzuri, lakini ukitaka kujifanya mzalendo ukaogea nao kiswahili basi wataanza kukupekuwa hadi kwenye mdomo, halafu wataanza kuomba chochote.

Wednesday, May 5, 2010

kwanini tunakuwa nyuma siku zote

unajuwa wakati mwingine mimi najiuliza kwanini tanzania tuko nyuma kimaendeleo ingawa nchi yetu imebarikiwa kwa kwa mali asiri nyingi: sio tu madini bali hata aridhi yenye lutuba, nafikiri tanzania inashika namba katika nchi zena alidhi zuri. Pamoja nahayo bado watanzania wengi ni masikini. Kweli tunapaswa kujiliza tatizo liko wapi? Kwa ufupi naweza kusema chanzo kikubwa cha matatizo ya watazania kiko mikononi mwao wenyewe, maana mtu huwezi kufanya kitu kimaja miaka nenda rudi ukategemea kwamba matokeo yatakuwa tafauti. Kwa mfano mtu unalima shamba la eka moja kila mwaka na unapanda maharegwe harafu unategemea kwamba siku moja hilo shamba lako litakuja kukupa mahitaji yako ya mahindi, mchele, nguo na kadharika. Nia yangu sio kuwadharau watanzania kwamba ni wachovu wa mawazo ila nichataka kuonyesha hapa nikwamba watazania kwa ujumula kuazia viogozi wa juu hadi mwanachi wa kawaida kama wanasiasa wetu wanavyo tuita sisi wakulima wa jembe la mkono kwamba ni wananchi wakawaida, tunahitaji kukaa chini natujiulize ni kipi tunakosea kwani nidhahili kuwa kwamba tulicho kuwa tunakifanya kwa miaka mingi sasa sio sahihi. Kwamaana hiyo tubadili mbinu zetu za kuleta maendeleo au tukubali kuwa umasikini ndio staili ya maisha tulio ichagua.