Saturday, June 26, 2010

hatakama umeukana utanzania bado wewe ni mtanzania

sasa tuna weza kuwekeza au kurudi kutowa changamoto nyumabani tanzania bila kisingizio kwamba oh mimi sio mtanzania tena. tanzania sasa iko kwenye process ya kupitisha sheria ya kuwa na uraia wa nchi mbili. Lakini swali ni kwamba hivi kweli watanzania wanao ishi nchi za nje wako tayari kurudi nyumbani kuwekeza au kutowa chagamoto kwa watanzania ambao hawajawahi kuwa na nafasi ya kutoka nje ya nchi? Mimi naamini kama watanzania wanao ishi nchi za nje wanao nafasi nzuri ya kuleta maendeleo tanzania kama wakiamua kubadilika na kujuwa kwamba nyumbani ni nyumbani hata kama kuna vumbi. wantazania wengi ambao hawajawahi kuishi nje ya nchi bado wana imani potofu kwamba wageni ni bora kuliko wenyeji. Kwa mfano mtu unakuta mhudumu anaona amuhudimie vuzuri mzungu kuliko mtazania mweusi. Mfano mzuri ni pale airport Dar ukitaka usisumbuliwe na wafanyakazi wa airport ni bora usiogea kiswahili ujifanye wewe ni mgeni ndio utahudumia vuzuri, lakini ukitaka kujifanya mzalendo ukaogea nao kiswahili basi wataanza kukupekuwa hadi kwenye mdomo, halafu wataanza kuomba chochote.

No comments:

Post a Comment